Kuhusu:

Zero UTI aims at decreasing the spread U.T.I among girls in secondary schools and the entire community.

Tatizo

Watu milioni 8.1 wanaugua UTI kulingana na takwimu za WHO 2017.

Kulingana na utafiti tuliofanya katika shule 5 za umma jijini Dar es salaam, tuligundua kuwa wasichana ndio kundi walioathirika zaidi na UTI kwa sababu ya vyoo ni vichache, vichafu na duni, na ukosefu wa mashuleni pamoja na elimu ya usafi wa kibinafsi. Hali hii inawafanya wasichana waone mara nyingi kuepuka kutumia vyoo siku nzima wakiwa mashuleni au wanalazimika kutumia vyoo duni. Hii imechangia wasichana kutokuenda shule, kuongezeka kwa idadi ya wanaoacha shule na wenye utendaji duni. Pia huwafanya wapate magonjwa mengine mabaya katika siku za usoni kama saratani ya shingo ya kizazi na magonjwa ya figo.

Tunachofanya

Kupitia jukwaa hili linalotokana na wavuti tunakuza uhamasishaji kwa wanafunzi na wadau muhimu kuhusu usafi wa kibinafsi na hali muhimu za maji na usafi wa mazingira mashuleni. Mfumo huo pia utawaalika wadau mbalimbali kuboresha hali ya WASH katika shule zilizochaguliwa.