Kudhibiti:

Tawaza njia sahihi

Jitawaze kuanzia mbele kwenda nyuma

Mara nyingi maambukizi ya kibofu cha mkojo husababishwa na E. coli, bacteria wa kawaida wanaioishi kwenye njia yako ya utumbo. Hii hukusaidia kuchimba chakula chako, lakini ukifuta kutoka kwa nyuma una hatari ya kuipaka nyama yako ya urethral. Halafu bakteria wanaweza kushikamana na ufunguzi wa urethra, kuzidisha na kusababisha UTI.

Badilisha Pedi Ndani ya Muda Mfupi

Wanawake hupaswa kubadili pedi zao kipindi cha hedhi mara kwa mara

Kuvaa pedi pekee hakusababishi maambukizi ya njia ya mkojo, bali kinachoendelea ndani au karibu na pedi yako huweza kusababisha maambukizi.

Mara nyingi pedi hutengenezwa na vifaa vya nyuzi bandia. Vifaa hivi vinaweza kutengeneza eneo mazingira mazuri kwa bakteria kuzaliana hasa kama pedi haiwezi kufyonza damu ya hedhi vizuri. Uwezo mdogo wa pedi kufyonza damu ya hedhi huongeza uwezekano mkubwa wa sehemu zako za siri na njia ya mkojo kuwa wazi kwa bakteria.

Maambukizi hutokea pale bakteria wakiwa karibu na njia ya mkojo na kuzaliana, na kusababisha maambukizi ya urethra, maarufu kama urethritis. Bakteria mara nyingi huenea hadi kwenye kibofu, na kusababisha maambukizi ya kibofu cha mkojo, maarufu kama cystitis. Bila kupata tiba, maambukizi yanaweza kuendelea kuenea kwenye njia ya mkojo, na kusababisha maambukizi katika figo.

Usafi wa nguo za ndani

Usichangie chupi na usivae chupi yenye unyevunyevu

Kuchangia chupi kunaweza kukupa maambukizo ya bakteria ya watu wengine, hivyo basi inamaanisha ikiwa ukichangia chupi na mtu mwenye bakteria wa E.coli kwenye sehemu za siri, inakupa hatari ya kuambukizwa UTI.

Epuka kuvaa chupi zenye unyevunyevu kwani joto na unyevu ni mazingira mazuri wa kuzaliana kwa bakteria

Kunywa Maji Mengi

Kunywa vimiminika kwa wingi hasa maji.

Kunywa maji mengi husaidia kusafisha njia ya mkojo kwa kuhahakikisha kuwa uta kukojoa mara kwa mara, na hivyo itawalazimu bakteria ya maambukizi kutoka kwenye njia yako ya mkojo kabla ya kuambukizwa.

Kunawa Mikono

Hatua tano za kunawa mikono kwa usahihi

Kuosha mikono yako ni rahisi, na ni njia mojawapo ya kuzuia kusambaa kwa vijidudu. Mikono safi inaweza kuzuia vijidudu kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na kwa jamii nzima — kutoka nyumbani kwako na mahali pa kazi hadi kwenye vituo vya utunzaji wa watoto na hospitali.

Fuata hizi hatua tano kila mara

Lowesha mikono yako na maji safi, yanayotiririka (ya joto au baridi), funga bomba, na paka sabuni.
Sugua mikono yako ili sabuni itengeneze povu, Sugua juu ya mikono, katikati ya vidole na chini ya kucha. Sugua mikono yako kwa kadri ya sekunde 20. Unaweza kuimba nyimbo ya happy birthday mara mbili na mda utakuwa umetimia.
Suuza mikono yako vyema na maji safi , yanayotirirka
Kausha mikono yako kwa taulo safi au kwa upepo
Unaweza kuwa msaada kwako mwenyewe na wapendwa wako kuwa na afya bora kwa kuosha mikono mara nyingi, haswa katika nyakati hizi muhimu ambapo kuna uwezekano wa kupata na kueneza vijidudu:

Kabla

  • Kabla na baada ya kuandaa chakula
  • Kabla ya kula chakula
  • Kabla na baada ya kumhudumia mgonjwa anayetapika au kuharisha
  • Kabla na baada ya kuhudumia kidonda

Baada

  • Baada ya kutumia choo
  • Baada ya kubadili nepi ya mtoto au kumsafisha mtoto aliyetumia choo
  • Baada ya kukamua pua, kukohoa au kupiga chafya
  • Baaada ya kushika mnyama, vyakula vya wanyama, au kinyesi cha wanyama
  • Baada ya kushika uchafu