Dalili:

Dalili za UTI’s

 • Kuwa na hali ya mkwamo wa mkojo
 • Kuwa na maumivu wakati ya kukojoa
 • Kuwa na hali ya mkojo kutoka toka kwa kiasi kidogo
 • Mkojo unaokuwa kama mawingu
 • Kuwa na mkojo wenye rangi nyekundu, wenye rangi kama pinki au rangi kama ya kokakola (kuwa na ishara ya damu kwenye mkojo)
 • Kuwa na mkojo wenye harufu kali

Dalili za kawaida zinazotokea kwa wanawake.

Wanawake wenye maambukizi ya chini ya njia ya mkojo wanaweza kuwa na maumivu ya fupanyonga. Hii ni pamoja na dalili zilizoorodheshwa hapo juu. Dalili za maambukizi ya juu ya njia ya mkojo zinafanana kwa wanawake na wanaume.

Dalili za kwaida zinazotokea kwa wanaume.

Dalili za maambukizi ya chini ya njia ya mkojo “UTI” kwa wanaume ni pamoja na maumivu ya rectum (rectal) pamoja na dalili ambazo zimetajwa hapo juu. Dalili za maambukizi ya juu ya njia ya mkojo kwa wanaume ni sawa na dalili zile zinazowakumba au zinazotokea kwa wanawake.
Maambukizi ya njia ya mkojo “UTI” hayatoi ishara na dalili mara kwa mara lakini maambukizi haya yanapotoa ishara na dalili zinaweza kujumuisha baadhi ya ishara na dalili zilizoorodheshwa hapo juu.

AINA ZA UTIs

Kila aina ya maambukizi ya “UTI” inaweza kutoa au kuonyesha ishara na dalili yake na hali hii itategemeanan na sehemu ambapo patakuwa na maambukizi hayo.

Sehemu ya maambukizi ya njia ya mkojo “UTI” Ishara na dalili
Urethra
 • Kuwa na maumivu wakati wa kukojoa
Kibofu
 • Shinikizo katika fupanyonga
 • Maumivu ya chini ya tumbo
 • Kukojoa mara kwa mara, na kuwa na maumivu wakati ya kukojoa
 • Mkojo kuwa na damu
Figo
 • Kuwa na maumivu ya juu ya upande kwenye figo
 • Kuwa na homa kali
 • Kuwa na hali ya kutetemeka
 • Kuwa na kichefuchefu
 • Kutapika